Karamu Ya Arusi Ya Mwana Kondoo Na Matukio Ya Enzi Za Mwisho

Marriage Supper of the Lamb- Swahili

UTAMBULISHO KUTOKA KWA BWANA
Wanangu, huyu ni Bwana wenu anayenena nanyi. Naja kwa upesi.
Kurudi kwangu kumewadia, Ni mlangoni. Naja! Jitayarisheni.
Ujumbe huu uliandikwa na binti yangu Susan akiwa kwa mfungo
wa siku arobaini, kwa ombi langu. Nilimleta mahali faragha ili aweze
kujinyima. Nilimpa maneno mengi niliyotaka yawajie ninyi wanangu.
Kwa hivyo aliyaandika jinsi nilivyo mwelekeza. Barua hizi zote zina
ujumbe maalum ambao mnahitajika kuusoma na kutafakari kwa
maana kurudi kwangu kumekaribia.
Ni Mimi Bwana na Mwokozi wenu,

Yahushua (Yesu Kristo)

Close up photo of white flowers on a grey background